13 Dec 2015

MSANII HUYU AMZAWADIA MKEWE SH BILIONI MBILI ZA KITANZANIA BAADA YA KUJIFUNGUA MTOTO WA KIUME, MTAZAME HAPA.


Picha kutoka maktaba.

STAA wa Hip Hop, Kanye West amefanya kufuru baada ya kutoa kiasi cha dola milioni 1 (zaidi ya bilioni 2 za Kitanzania) ikiwa ni shukrani kwa mke wake kumpatia mtoto wa pili.
Kanye alifanya hivyo hivi karibuni ikiwa ni siku chache tangu Kim ajifungue mtoto wa kiume aliyemuita jina la Saint West.

Kim Kardashian.

Kwa mujibu wa Jarida la People la Marekani, Kanye humwambii chochote juu ya ujio wa mtoto wake huyo na kwamba amekuwa akimhudumia Kim kama vile malkia.
“Tangu Kim amejifungua amekuwa ni mchovu sana kwani bado anamaumivu makali ambayo hayaelezeki na ndiyo maana Kanye anafanya kila liwezalo awe karibu na Kim na kumsaidia kila kitu kama malkia anavyofanyiwa,” iliandika sehemu ya jarida hilo.
Kim na Kanye walifunga ndoa Mei mwaka huu pande za Paris, Ufaransa na kisha kuhamishia sherehe pande za Italia. Wawili hao wamebahatika kupata watoto wawili ambapo wa kwanza ni wa kike anaitwa North West na wa pili wakiume, Saint West.
kanye-west-treats-kim-karda
Kanye West na mkewe Kim Kardashian.



0 comments:

Post a Comment