31 Oct 2015

BASI LA PRINCESS MURO LAPATA AJALI MIKUMI MKOANI MOROGORO NA KUUA WATU SITA,HABARI KAMILI HAPA PAMOJA NA PICHA.

Watu sita wamefariki dunia papo hapo baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya toyota Noah iliyo kuwa ikitokea mikumi kwenda Morogoro  kupasuka tairi ya mbele upande wa kulia na kuanza kuyumba barabarani kisha kugongana uso kwa uso na basi mali ya kampuni ya Princes Muro katika eneo la mbuga ya taifa Mikumi.

Picha iki onesha basi la Princes Muro mamoja na mabaki ya Noah 

Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Lenard Paulo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema ajali hiyo  imetokea majira ya saa tano asubuhi ndani ya hifadhi ya taifa mikumi kilometa tatu kufika geti la kutokea ndani ya hifadhi hiyo nakusababisha ajali hiyo iliyo sababisha vifo hivyo vya watu sita wakiwemo wanawake wawili na wanaume wanne na miili imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.

Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Lenard Paulo

Aidha kamanda Paulo amewataka madereva wanao endesha vyombo vya moto kuwa makini na kuendesha magari kwa mwendo wa taratibu hasa wanapokuwa katika maeneo ya mbuga za taifa kwani sheria haziruhusu mwendo kasi ambapo amesema dereva wa basi anashikiliwa na jeshi la Polisi.

Moja kati ya mabasi ya Princes Muro

Source: ITV

0 comments:

Post a Comment