Dkt. John Pombe Magufuli alipokutana uso kwa uso na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana alikutana uso kwa uso na aliyekuwa mpinzani wake mkubwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa.Viongozi hao walikutana katika maadhimisho ya Jubilei ya Dhahabu ya Miaka 50 ya Ndoa ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa yaliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam na kufuatiwa na hafla iliyofanyika nyakati za mchana katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa uliopo kando ya kanisa hilo.
Jubilei hiyo ilihudhuriwa na viongozi wengine mbalimbali wakiwemo Mke wa Rais wa Rais Magufuli Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume, Mke wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere, Mawaziri Wakuu Wastaafu Mhe. Cleopa Msuya, Dkt. Salim Ahmed Salim na Jaji Joseph Warioba.
Ikumbukwe: Katika uchaguzi huo uliofanyika mwaka, Lowassa aliyekuwa akiwakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) alipata zaidi ya kura milioni sita huku Rais Magufuli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akishinda kwa kupata kura zaidi ya milioni nane.
Cheki picha zaidi hapa chini...
Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa
Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakikata keki
0 comments:
Post a Comment