Nyumba walimokua wakiishi majambazi eneo la vikindu wilaya ya Mkuranga
Nyumba walimokua wakiishi majambazi eneo la vikindu wilaya ya Mkuranga mkoani pwani imekutwa na matundu ya risasi zaidi ya 50, kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu.Kwa mujibu wa kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salamu, Simon Sirro amesema ifikapo jumanne ripoti kamili itatolewa juu ya tukio zima lililotokea wilayani humo.
Ikumbukwe kua Mapigano makali yalikua yakiendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, mapigano hayo yalitokea eneo la Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani mnamo tarehe 25 mwez huu na yalidumu kwa usiku mzima.
Chanzo: gazeti la mwananchi online
0 comments:
Post a Comment