15 May 2016

MWANA FA NA AY WAIKABA TIGO, WADAI FIDIA BILIONI 2 KWA WIZI WA KAZI ZAO.


Image result for tigo
Logo ya tigo

Hamisi Mwinijuma "Mwana FA" na Abwene Yesaya "AY" wadai fidia ya bilioni 2 za kitanzania kwa kampuni ya huduma ya simu ya TIGO baada ya kampuni hiyo kutumia kazi za wasanii hao (muziki wao) bila ridhaa wala makubaliano toka kwa wamiliki, Mwana FA na AY.
 
Abwene Yesaya "AY"

Kazi ambazo kampuni ya TIGO ilizitumia ni pamoja na wimbo uitwao "USIJE MJINI" wa Mwana FA pamoja na wimbo uitwao "DAKIKA MOJA" wa AY.

Hamisi Mwinijuma "Mwana FA"

Wakati huo huo rufaa waliyotaka kakata kampuni ya TIGO dhidi ya wasanii hao yakutaka isiwalipe kitita hicho cha pesa imegonga mwamba baada ya kuwekewa kipingamizi.

source:blog ya wanachi

0 comments:

Post a Comment