
Picha iki onesha basi la Princes Muro mamoja na mabaki ya Noah
Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Lenard Paulo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa tano asubuhi ndani ya hifadhi ya taifa mikumi kilometa tatu kufika geti la kutokea ndani ya hifadhi hiyo nakusababisha ajali hiyo iliyo sababisha vifo hivyo vya watu sita wakiwemo wanawake wawili na wanaume wanne na miili imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.

Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Lenard Paulo
Aidha kamanda Paulo amewataka madereva wanao endesha vyombo vya moto kuwa makini na kuendesha magari kwa mwendo wa taratibu hasa wanapokuwa katika maeneo ya mbuga za taifa kwani sheria haziruhusu mwendo kasi ambapo amesema dereva wa basi anashikiliwa na jeshi la Polisi.

Moja kati ya mabasi ya Princes Muro
Source: ITV
0 comments:
Post a Comment