17 Feb 2016

SERIKALI YAJIVUNIA CHUO KIKUU (UDOM), BAADA YA WANAFUNZI WAHANDISI WA NISHATI NA MADINI KUTEMBELEA BUNGE.HABARI KAMILI HAPA.

Serikali kupitia spika wa bunge ndugu Jobu Ndugai amesema serikali inajivunia uwepo wa chuo kikuu cha dodoma (UDOM) kwani ni chuo pekee kilicho jengwa kwa fedha za serikali.

Spika wa bunge ndugu Jobu Ndugai.

Alisema maneno hayo mnamo tarehe 1 mwezi wa pili mwaka huu alipokuwa akiwatambulisha na kuwakaribisha wageni waliokua wametembelea bunge siku hiyo, ambao kati ya hao walikuwa ni wanafunzi wahandisi wa nishati na madini(mining engineers, mineral processing engineers na petroleum engineers) wa mwaka wa nne kutoka chuo kikuu cha dodoma (UDOM), kitivo cha sayansi ya dunia (college of earth sciences, COES).
Aidha spika huyo wa bunge aliwahasa wanafunzi hao kuwa wawakilishi na wawajibikaji sahii katika jamii zao na ata kazini baada ya kumaliza masomo yao chuoni.
Wanafunzi wahandisi wa nishati na madini wa mwaka wa nne kutoka chuo kikuu cha dodoma (UDOM), kitivo cha sayansi ya dunia (college of earth sciences, COES).


CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)

0 comments:

Post a Comment