Teknolojia hiyo ya uundaji wa Roboti sasa imeleta hofu katika jamii kwenye swala la ajira maana imeonekana shuguli mbalimbali hasa viwandani itafanywa na hivi vifaa Roboti au Mashine.
Uko nchini Uingereza, takribani asilimia 35 (35%) ya ajira ziko hatarini kuchukuliwa na hizi Mashine katika miaka ishirini ijayo kulingana na utafiti uliofanywa katika chuo cha Oxford na Deloitte.
Utafiti huo unadai.shuguli ambazo zitakua zinafanywa na Roboti hao ni kama vile shughuli za viwandani, shughuli za kidaktari,udereva taxii na wahudumu wa migahawa.
Na uko nchini china, kuna kiwanda cha kwanza kinacho tengenezwa kiitwacho Dongguan ambacho kinategemewa kuchukua Maroboti kama wafanyakazi.
Kama mtanzania, kijana mwenye nguvu, hali na uwezo wa kufanya kazi, una mtazamo upi juu ya kukua kwa teknolojia hii ya Roboti?
0 comments:
Post a Comment